Phone: +255 24 2235567
email: dppznz@dppznz.go.tz

Search
Close this search box.

OFFICE OF THE DIRECTOR OF PUBLIC PROSECUTIONS

Transactional Organised Crime Unit

IDARA YA MAKOSA YA KIUCHUMI NA YANAYOVUKA MIPAKA

Idara inawajibika kwa Mkurugenzi wa Mashtaka na ina majukumu yafuatayo:

  1. Kusimamia Uendeshaji Mashtaka katika makosa yanayohusiana na Fedha, Uchumi, Dawa za Kulevya, Uhalifu wa Kimtandao na Makosa yanayovuka mipaka.
  • Kusimamia utendaji wa Divisheni zilizo chini ya Idara, ambazo ni Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Divisheni ya Makosa Utakatishaji Fedha na Utaifishaji wa Mali za Wahalifu, Divisheni ya Makosa ya Dawa za Kulevya na Uhalifu wa Kimtandao, Divisheni ya Makosa ya Kupangwa na yanayovuka Mipaka na Kitengo cha Masuala ya Fedha na Benki.
  •  Kuhakikisha Wanasheria wanaambatana na sera na miongozo iliyokupitishwa pamoja na kuwasilisha taarifa za utendaji kila baada ya miezi mitatu.
  • Kuzifanyia uchambuzi hukumu au maamuzi madogo ya Mahakama pamoja na kuandaa nyaraka zinazohitajika katika hatua ya Rufaa, Mapitio au Marejeo ya Mienendo ya Kesi pale inapohitajika. Pamoja na Kusimamia Rufaa za kesi husika zilizofunguliwa katika Mahakama.
  • Kuwasilisha kwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka taarifa na nyaraka muhimu za kesi iliyoisimamia katika hatua ya usikilizwaji au Rufaa katika Mahakama Kuu pale kesi hiyo itakapoendelea na hatua ya Rufaa katika Mahakama ya Rufani Tanzania.
  • Kuishauri Serikali, Wizara, Idara pamoja na Taasisi nyengine kuhusiana na makosa ya Kifedha, Uchumi, Dawa za Kulevya, Uhalifu wa Kimtandao na Makosa yanayovuka mipaka.
  • Kutoa Maelekezo na Ushauri kwa Taasisi zinazofanya Upelelezi wa Makosa ya Fedha Uchumi, Dawa za Kulevya, Uhalifu wa Kimtandao na Makosa yanayovuka mipaka
  • Kusimamia Mikataba ya Kimataifa na Kikanda pamoja na nyenzo nyengine ambazo zinajikita katika kuzuia, kudhibiti pamoja na kuendesha Mashtaka katika makosa yanayohusiana na Fedha, Uchumi, Dawa za Kulevya, Uhalifu wa Kimtandao na Makosa yanayovuka mipaka
  1. Kufanya Utafiti, Mapitio na kuandaa mapendekezo kuhusu ubora na nafasi ya Sheria mbali zinazohusiana na makosa ya Fedha, Uchumi, Dawa za Kulevya, Uhalifu wa Kimtandao na Makosa yanayovuka mipaka.
  • Kuandaa Mpango Kazi na Miongozo inayohusu uendeshaji Mashtaka katika Fedha, Uchumi, Dawa za Kulevya, Uhalifu wa Kimtandao na Makosa yanayovuka mipaka.
  • Kusimamia ufatiliaji wa Mali za Wahalifu pamoja na kuandaa taratibu za kutaifisha mali hizo kwa mujibu wa Sheria.
  • Kusimamia utekelezaji wa Miongozo na Sheria ya Mashirikiano ya Kikanda na Kimataifa (Mutual Legal Assistance) pamoja na zinazohusu kusafirisha Wahalifu (Extradition laws).
  • Kuanzisha na Kuendeleza Mashirikiano na Taasisi za Kikanda na Kimataifa zinazojikita katika kuzuia, kudhibiti makosa yanayohusiana na yanayopangwa na yanayovuka mipaka.
  • Kuandaa ripoti ya kila mwezi, miezi mitatu na mwaka ya utendaji wa Idara na kuziwasilisha katika Idara ya Uratibu wa Mashtaka ambayo itawasilisha ripoti hizo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka.
  • Kushajihisha mashirikiano na wadau wa Haki Jinai.

Kufanya kazi nyengine Idara itakazopangiwa na Mkurugenzi wa Mashtaka.