Divisheni ya Mipango na Takwimu
Divisheni hii ina jukumu la kusimamia mipango na takwimu za Ofisi, kuhakikisha upangaji bora wa rasilimali, uchambuzi wa data, na utoaji wa taarifa za kitaalamu kwa madhumuni ya uongozi na uamuzi.
Utangulizi wa Divisheni
Divisheni ya Mipango na Takwimu ina jukumu muhimu la kusimamia mipango na takwimu za Ofisi ya DPP Zanzibar. Divisheni hii inalenga kuhakikisha kwamba shughuli zote za taasisi zinaendeshwa kwa mujibu wa mipango iliyokusudiwa, bajeti inatumiwa kwa ufanisi, na takwimu zinazotolewa ni sahihi na zinatumika kwa kutengeneza maamuzi ya kiuchumi.
Lengo kuu la divisheni hii ni kutoa mwongozo wa kimaendeleo, kufanya uchambuzi wa takwimu wa kitaalamu, na kuhakikisha utoaji wa taarifa sahihi kwa ajili ya uongozi na maamuzi ya kitaasisi.
Maeneo ya Mkusanyiko
Divisheni hii inashughulikia nyanja kuu tatu za mipango na uchambuzi wa takwimu:
Uandaji, kuratibu na ufuatiliaji wa mipango ya kazi, mikakati ya muda wa kati, na bajeti za taasisi kwa kipindi cha mwaka.
Uratibu wa utayarishaji, utekelezaji na ufuatiliaji wa bajeti ya Afisi, kuhakikisha matumizi bora ya fedha kwa mujibu wa mipango ya kazi.
Ukusanyaji, uchambuzi na utafsiri wa takwimu na taarifa za kiuchumi kwa ajili ya utoaji wa maamuzi ya kitaalamu na taarifa za kitaasisi.
Majukumu ya Divisheni
Divisheni ya Mipango na Takwimu ina majukumu yafuatayo:
Kukusanya taarifa na kutayarisha Mpango Kazi wa mwaka na Mpango Mkakati wa muda wa kati wa Afisi.
Kuratibu utayarishaji na utekelezaji wa Bajeti ya Afisi.
Kukusanya taarifa za Miradi/programu na Mipango kazi ya Afisi.
Kutoa ushauri wa kitaamu juu ya kutekelezwa Mpango Mkakati wa taasisi na kutayarisha Bajeti.
Kukusanya taarifa za mapitio ya utekelezaji kwa kipindi cha muda wa kati na mwaka.
Kuratibu utekelezaji wa maamuzi ya Serikali juu ya masuala ya mipango na uongozi wa masuala ya kiuchumi.
Kuchambua na kutafsiri (interpret) takwimu na taarifa mbali mbali za kiuchumi.
Kubuni Mipango ya utafiti na mapendekzo ya fedha kwa ajili ya utekelezaji wa tafiti.
Kuratibu, kuongoza na kuangalia ubora wa mchakato wa ukusanyaji takwimu na taarifa.
Kuratibu na kusimamia namna bora ya kutafsiri takwimu na taarifa.
Kuratibu usambazaji wa takwimu na taarifa.
Kufanya uchambuzi na kutayarisha taarifa kwa ajili ya usambazaji, uhifadhi na kuhakikisha taarifa za mwisho za uchambuzi zinapatikana kwa watumiaji kwa njia ya tovuti na maktaba.
Kuwasiliana na wadau wote husika na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali katika kutayarisha, kutafsiri, kuimarisha na kusambaza takwimu na taarifa.
Kuwajibika katika kutoa takwimu, utaalamu, katika maeneo husika kwa mujibu wa maelezo ya viwango vinavyohitajika kitaifa na kimataifa.
Kufanya kazi nyengine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
Umuhimu wa Mipango na Takwimu
Divisheni ya Mipango na Takwimu ina jukumu muhimu katika kuhakikisha ufanisi na uadilifu wa shughuli za taasisi. Kwa kutoa mipango sahihi, uchambuzi wa kitaalamu wa takwimu, na usimamizi bora wa bajeti, divisheni hii inachangia kwa kiasi kikubwa katika kufikia malengo ya taasisi. Mipango bora na takwimu sahihi ni msingi wa maamuzi ya kiuchumi na uongozi bora, na hivyo divisheni hii inakuwa kiini cha mafanikio ya taasisi kwa ujumla.